Dili la usajili wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ureno na klabu ya Benfica Gonçalo Manuel Ganchinho Guedes, aliyekua anawindwa na Man Utd limeota mbawa.

Jana Rais wa klabu ya Benfica Luís Filipe Vieira Ferreira, aliripotiwa kufunga safari kuelekea mjini Manchester nchini England, kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya uhamisho wa mshambuliaji huyo, lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo.

Guedes amegoma kujiunga na Man Utd, kwa shinikizo la kutaka asajiliwe na mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, ambao tayari wameshaonyesha nia ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

Guedes mwenye umri wa miaka 20, ameripotiwa kuwa katika harakati za kuelekea mjini Paris, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa PSG yatakayotoa mustakabali wa maslahi yake binafsi, kabla ya ada yake ya uhamisho ya Euro milioni 30 haijalipwa.

Kutokana na mambo hayo kuharibika, bado Man Utd wana mpango wa kufanya biashara na klabu ya Benfica ndani ya juma hili, na sasa wamewageukia Victor Lindelof (Beki Wa Kati) na Nelson Semedo (Beki Wa Kushoto).

Man Utd wamepanga kuwasajili wachezjai hao wawili kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 30.

Uhamisho wa wawili hao unatarajiwa kukamilishwa ndani ya saa 24 zijazo, kwa kuhofia mipango iliyowekwa na klabu za Atletico Madrid, FC Bayern Munich pamoja na FC Barcelona ambao wamejipanga kuingilia kati dili hilo.

Young Killer: Muziki wa Hip pop utengewe muda
Philippe Coutinho Kuwekewa Uzio Anfiled