Klabu ya AS Monaco ipo katika harakati za mwisho za kukubaliana na Man Utd ili kukamilisha dili la kumuuza mshambuliaji wa kifaransa Anthony Martial ambaye anaonekana huenda akawa msaidizi mzuri kwenye safu ya ushambuliaji huko Old Trafford.

AS Monaco wametajwa kukubali dili la paund million 36 kama ada ya usajili wa mshambuliaji huyo na huenda hii leo mipango yote ikakamilishwa kabla ya dirisha ya usajili halijafunmgwa rasmi.

Anthony Martial mwenye umri wa miaka 19 amekua na kiwango cha kustaajabisha katika kikosi cha AS Monaco na mara kadhaa ameshaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps.

Martial, alikuwepo kikosini mwishoni mwa juma lililopita wakati AS Monaco walipokubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya mabingwa watetezi Paris Saint-Germain.

Hata hivyo usajili wa mshambuliaji huyo huenda ukaipa gharama kubwa Man Utd licha ya kutajwa utagharimu paund million 36, kutokana na masuala mengine ya uhamisho.

Pound million 22 za mambo mengine ambayo hayakutajwa hadharani kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo, zitaifanya Man Utd kutoa kiasi cha paund million 58.

Kama itakuwa hivyo Martial, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kwa kiasi kikubwa na Man Utd, baada ya usajili mkubwa kufanyika Old Trafford msimu uliopita uliomuhusisha mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina, Angel Di Maria wakati akitokea Real Madrid.

“Msidanywe Kuhusu Sheria Ya Makosa Ya Mtandao”
Januzaj Apigwa Bei Ujerumani