Manchester United wamethibisha kuumia kwa beki wa pembeni Luke Shaw wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliowakutanisha na mabingwa wa soka nchini Uholanzi PSV Eindhoven.

Luke Shaw alipatwa na dhorubwa la kuvunjika mguu katika dakika ya 15 ya mchezo huo baada ya kukabiliana na beki PSV ambaye ni raia wa nchini Mexico, Hector Moreno.

Meneja wa Man Utd, Louis Van Gaal amethibitisha kuumia kwa beki huyo mwenye 20, alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa kwenye uwanja wa Philips Stadion, usiku wa kuamkia hii leo.

Van Gaal, amesema beki huyo alionekana dhahir amevunjika mguu akiwa uwanjani hatua ambayo ilipelekea kutolewa nje ya uwanja akiwa katika uangalizi maalum wa matabibu na watu wa huduma ya kwanza.

Amesema baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali, imebainika Luke Shaw amevunjika mara mbili mguu wake wa kulia na itamchukua zaidi ya miezi sita mrefu kurejea tena uwanjani.

Kufutia tukio hilo, mchezo wa PSV dhidi ya Man Utd, ulilazimika kusimama kwa muda wa dakika 10 kupisha taratibu za huduma ya kwanza alizokua akipatiwa Luke Shaw uwanjani, huku kila mchezaji akionekana amejawa na simanzi.

Katika mchezo huo Man Utd walikubali kupoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.

Ronaldo Akandamiza Tatu Champions League
Ni Kusuka Ama Kunyoa Kwa TP Mazembe