Uongozi wa Manchester United umekataa kukutana na mawakala kwani wanaamini kuwa wanajaribu kuwatafutia wateja wao kuchukua nafasi ya Erik ten Hag, kwa mujibu wa ESPN.

Ten Hag alipunguza shinikizo kwenye nafasi yake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Luton Town Jumamosi (Novemba 11) katika mchezo wa mwisho wa United kabla ya mapumziko ya kimataifa ya Novemba hii.

Licha ya kupoteza mara tisa katika mechi 18 za msimu mpya, Mholanzi huyo anabaki kuaminiwa na viongozi wakuu wa klabu baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England na kushinda Kombe la Carabao msimu uliopita.

Vyanzo vimeiambia ESPN kwamba wakuu wa United wamechanganyikiwa na majaribio ya mawakala kushinikiza makocha kuwania nafasi ya Ten Hag.

Mmoja wa wakala wa kocha mashuhuri, ambaye hayuko kazini, aliahirisha mkutano ulioratibiwa kwa sababu ya wasiwasi kwamba mazungumzo hayo yasingekuwa na matokeo chanya.

Mabosi wa United wanaamini kuwa kumekuwa na dalili za maendeleo katika kipindi cha juma moja ambapo timu ya Ten Hag imezishinda Fulham na Luton kwenye Ligi Kuu, lakini walifungwa 4-3 na FC Copenhagen kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Lakini inakubalika kwamba uwekezaji unaokuja wa Sir Jim Ratcliffe utaleta uhakika katika viwango vyote vya klabu mara tu utakapothibitishwa.

Ratcliffe, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kemikali ya INEOS, anakaribia kukubaliana na ununuzi wa hisa asilimia 25 za klabu hiyo.

Kwa hili tumepakwa mafuta kwa Mgongo wa Chupa - Bwege
Mnagombana kila siku, haina faida - Waziri Mkuu