Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Chile Reinaldo Rueda ametangaza kikosi, na kumuacha mshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez kufuatia ombi alilolipokea kutoka kwenye uongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford.

Manchester United waliwasilisha ombi katika shirikisho la soka nchini Chile, la kutaka mshambuliaji huyo aachwe katika kipindi hiki, ili aweze kupata nafasi ya kupumzika, hasa baada ya kupona majeraha ya mwili ambayo yalimsababishia kukosa mchezo dhidi ya Brighton and Hove Albion majuma mawili yaliyopita.

Katika kikosi kilichotajwa na kocha Reinaldo Rueda, kiungo wa FC Barcelona Arturo Vidal ni miongoni mwa wachezaji walioitwa, kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Japan na Korea Kusini itakayochezwa Septemba 6 na 10.

“Hatua ya kutomuita Sanchez imetokana na ombi nililolipokea kutoka Manchester United, wamenitaka nimpe muda ili aweze kuwa na utimamu mzuri wa mwili,” alisema kocha wa Chile, Rueda.

“Kwa mujibu wa taarifa zilizoambatanishwa kwenye ombi la Man Utd, imeelezwa kuwa, Sanchez kwa sasa anaendelea vizuri, lakini kulikua na hofu huenda angetonesha sehemu alizokua akiumwa katika majuma mawili yaliyopita.”

Image result for sanchez left out by chile at man united's request

“Ninaendelea kuuheshimu mchango wa Sanchez katika timu ya taifa, na muda utakapowadia nitamuita ili aje kusaidiana na wachezaji wengine kiosini, lakini kwa sasa tumpe muda.”

Timu ya taifa ya Chile ambayo haikupata nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia 2018, itacheza dhidi ya Japan mjini Sapporo kabla ya kupambana na Korea Kusini mjini Suwon.

Video: Haya ndio magereza yenye ulinzi mkali zaidi duniani
Wasiliana na bosi wako wa zamani kwa njia hizi 5 rahisi