Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Erasmus Hojlund atachelewa kurudi dimbani kutokana na matatizo ya mgongo baada ya kugundulika kwenye vipimo vya afya.
Uchunguzi wa kipimo cha MIR kimeonyesha mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 72 milioni amegundulika ana tatizo la mgongo ambalo linaweza kusababisha msongo wa mawazo.
Hojlund mwenye umri wa miaka 20, ameondolewa kwenye kikosi kwa ajili ya mechi mbili za ligi za kwanza dhidi ya Wolves na Totenham kutokana na jeraha hilo alilopata wakati anakipiga Atalanta.
Kwa mujibu wa ripoti, Hojlund anahitaji wiki chache za kupumzika na kuwa fiti zaidi kabla ya kurejea dimbani kukiwasha.