Mtayarishaji mahiri wa muziki hapa Bongo na mmiliki wa studio za Combination sound, Man Walter amefunguka na kutaja sababu ambayo inamfanya msanii wa muziki Alikiba kuchelewa kutoa kazi zake kama ambavyo anatupiwa lawama hiyo kutoka kwa mashabiki wake wengi wanaomkubali na kupenda kazi yake.

Man Walter alipofanya mahojiano amesema utaratibu wa Alikiba kufanya kazi ni wa taratibu sana amesema hana haraka ya kufanya mambo, lakini pia sio msanii ambaye anawekeza pesa nyingi kwenye muziki wake wala akiba ya nyimbo kwenye stoo yake kama ilivyo kwa wasanii wengine.

”Utaratibu wake wa kufanya kazi uko ”slow” sana sio msanii ambaye yupo ”sharp” na sio msanaii ambaye anawekeza kwenye kazi yake, kwanza uwekezaji wa kipato na uwekezaji wa kuwa na stock ya nyimbo, mimi ndio nilikuwa namfundisha kuwa na stock, na alikuwa ni muoga wa kujipambana” amesema Man Walter.

Aidha ameongezea kuwa yeye amekutana na Alikiba kipindi ambacho alikuwa anahitaji msaada kwani alikuwa tayari ameshatoka kwenye reli ya muziki.

Pia ameongezea kuwa ngoma yake ya Dushelele aliyomtengenezea ndio ngoma iliyomrudisha kwenye reli kwani ngoma hiyo ilikuwa na baraka nyingi na ndiyo ngoma ya kwanza iliyompa tuzo na kufanya watu waanze kumuelewa na kuanza kuzikubali kazi zake.

Aidha Man Walter amekuwa mtayarishaji mzuri wa nyombo ametengeneza nyimbo mbalimbali za Alikiba zilizofanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki ikiwemo, Seduce me, iliyofanya vizuri baada ya kukaa kitambo kirefu zaidi ya mwaka bila kuachia ngoma yeyote.

Ngoma zake nyingine Alikiba alizotayarisha chini ya Man Walter ni Mvumo wa radi, mwambie sina aliyofanya na king music, mbio, pamoja na mshumaa na nyingine nyingi.

 

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333
Ukame Australia: Maelfu ya Ngamia kuuawa