Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano ya Simba SC Haji Sunday Ramadhana Manara, amempongeza mlinda mlango wa klabu hiyo Aishi Salum Manula kufuatia kiwango alichokioneksha kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Libya uliochezwa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Mchezo huo uliokua wa kukamilisha ratiba kwa kundi J ushuhudia Taifa Stars ikichimoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na mshambuliaji Simon Msuva, kipindi cha kwanza.

Manara amempongeza Manula kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kusisitiza bado anaendelea kuamini mlinda mlango huyo anaendelea kuwa na sifa za kipekee katika bara la Afrika kwa sasa.

Manara amaeandika: Guys huyu kipa kwa sasa yupo ktk kiwango bora sana na ndio maana si ajabu klabu kubwa Afrika kumzungumzia.

Niliwahi kumwambia mara kadhaa wakati ule Simba au Timu ya Taifa ikifungwa,na yy kuwa Bangusilo wa kulaumiwa,,kwamba ww ni kipa bora mno ila kinachokuponza ni huo muonekano wako tu,,Coz makosa yako ni genuine kwa makipa wote duniani!!

Leo Aishi upo ktk top na licha ya kudaka sana pia unafanya saves za hatari iwe Kwa Simba au Kwa Stars

Kwangu mm Aishi ndio MVP wangu wa msimu huu so far..

Muhimu kamatia hapo hapo,,soon utaimbwa Afrika nzima.

Bibi wa Barack Obama afariki dunia
Waziri Mkuu wa Armenia ajiuzulu