Mkuu wa idara ya habari na mawasilino ya Simba SC Haji Sunday Manara, amempongeza beki Kelvin Yondan kwa hatua ya kusajiliwa na Namungo FC, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Imefahamika kuwa Namungo FC imemsajili beki huyo wa timu ya taifa (Taifa Stars), akiwa mchezaji huru baada ya kuachwa na Young Africans mwishoni mwa msimu 2019/20.

Manara amempongeza Yondani ambaye aliwahi kuitumikia Simba SC, kupitia ukuarasa zake za mitandao ya kijamii (Facebook na Instagram), huku akimpa sifa zote kupitia umahiri wake uwanjani.

“Senior Stoper, Defender la nchi, Mkoba wa Taifa, Sentahafu Bora kabisa, nimearifiwa deal yako ya kuanza kutumikia Namungo fc kwenye Caf competition Msimu huu imekamilika,”

“Kila la kheri Mwambaaaaaa!!”

“Hadhi yako ww ni kucheza michuano mikubwa mikubwa.” Ameandika Manara.

Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwa washindi wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo limechukuliwa na Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Baraza: Simba walituzidi mbinu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 21, 2020

Comments

comments