Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara ameiomba TFF kumtoa kifungoni msemaji wa watani wao wa jadi, Yanga SC, Jerry Muro.

Muro alipigwa pingu ya mwaka mmoja kutoshiriki soka na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 3, adhabu iliyotolea na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kumkuta na hatia ya kutoa lugha za uchochezi, kupingana na maagizo ya Shirikisho hilo pamoja na kukaidi agizo la kulipia faini ya shilingi milioni 5.

Manara amekutwa na upweke wa kiushindani katika tasnia yake na ameamua kutumia mtandao wa Instagram kumuomba Rais wa TFF, Jamal Malinzi kumfikiria na kumsamehe mtani wake huyo ili waendelee kubadilishana tambo, majigambo na uzoefu.

JERRY MURO 00

Hivi ndivyo alivyoandika:

Kwako Rais wa TFF,

Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi

kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini,

kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba.

Nimekaa nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambae TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na teyari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake,

Nnajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,

Nnafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini yale yashapita na bnafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba,

Tunamiss rikaka zake zinazoongeza ushabiki na utani wetu wa jadi. kwangu Mh Rais nna hakika utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru,

ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaid duniani.

Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka. Wako

HAJI MANARA

Magufuli asimulia rozali ya ‘sister’ ilivyompa ushindi wa urais
Tanzia: Mwimbaji Mkongwe George Michael afariki akirekodi filamu