Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara ameendelea kusisitiza kuitetea klabu hiyo dhidi ya yoyote atakaeichafua.

Hii si mara ya kwanza kwa Manara kuipambania Simba SC, huku akiahidi kufanya lolote ili klabu hiyo kongwe Afrika Mashariki na Kati iwe salama.

Manara ameandika ujumbe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo ameeleza namna atakavyoendelea kuitetea Simba SC dhidi ya maadui.

Manara ameandika: Sometimes naweza kuonekana mkorofi na kuonekana mtu mtata ,,lakini wanaonijua vzuri wanafahamu mm sio mkorofi ila sio mtu wa kukubali kukaa kimya pale tassisi iliyonipa majukumu ikichezewa,,na ndio maana huwa nakaa kimya nikishambuliwa binafsi lakini sio Simba

Simaanishi tusikosolewe lakini tusionewe na kusemwa hovyo hovyo kwa Wachezaji wetu au Makocha na hata Viongozi wetu,,tunahitaji heshma tunayostahili kama klabu !!

Kuna kasumba imejengeka ya kwamba unaweza kuzusha lolote kwenye mpira na hususan kwetu na usifanywe lolote,,hilo kwa Simba mtanisamehe ndugu zangu,,sitamuangalia mtu usoni kwa sababu ww ni fulani ,,otherwise amua kuwa mtani wetu utucharure utakavyo ,,

Nimeamua kuandika haya mjue dhamira yangu ya kuilinda image ya Simba,,tunazo standard tulizoziset ili kufikia malengo yetu ,,hatutakubali kuanzia sasa tuchezewe kama mlivyo nyinyi msivyo tayari kuchezewa taasisi zenu mnazofanyia kazi ,,,,

Tukosoeni pale tunapovurunda lakini msiseme uongo au uzushi kwa maslahi yenu,,hilo subirini sie tuondoke lakini now HATUTAKUBALI TENA !!

Andiko hili fupi halina uhusiano na lolote liliotokea hv karibuni ni ktk kuwekana sawa tu Wakulungwa wenzangu

Azam FC yatinga Nusu Fainali ASFC
Ajinyonga kwa tuhuma za kuiba Shilingi 5000