Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Haji Sunday Manara amekubali matokeo ya kufungwa 1-0 na Young Africans leo Jumamosi (Julai 03).

Young Africans iliokuwa mgeni wa Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam imepata ushindi huo kupitia kwa kiungo wake Zawadi Mauya dakika ya 11 kipindi cha kwanza.

Manara ambaye alikua na uhakika wa kuona kikosi cha Simba SC kinaibuka na ushindi, amekubali matokeo kwa kuandika ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii (Instagram na Facebook).

Manara ameandika: “Alhamdulillah”

“Tumefungwa na Team iliyocheza kimbinu vema zaidi yetu na bahati kubwa kwao,,,,”

“Hatukuwa Simba first half but hyo ndio football”.

Jumatano (Juni 30) Manara alipozungumza na waandishi wa habari na alisema: ” Tuna wachezaji kama Chama, Bwalya, Bocco, Tshabalala, Kapombe, Taddeo, Onyango, halafu tunakutana na kikundi cha watu kilichokutana, Kama marefa watachezesha vizuri tutaibuka na ushindi usiopungua mabao matatu, licha ya kuwa heshima ya mpinzani lazima itakuwepo Kama ambavyo huwa wanacheza na timu zingine.”

Licha wa kupoteza dhidi ya Young Africans, Simba SC inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa alama 73 huku watani zao wakifikisha alama 70.

Uchambuzi wa Simba Vs Young Africans
Samatta achukuliwa 'Jumla Jumla' Fenerbahçe