Msemaji wa Klabu ya Soka ya Simba, Haji Manara amesema kuwa anampango wa kugombea urais na anaamini atafanikiwa.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio kilichopo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kazi zake anazofanya sasa zimemfanya apate hesima kubwa, kitu ambacho kinampa ujasiri wa kufikia uamuzi huo.

“Unajua mimi nakwenda kuwa rais wa nchi siku moja, mimi nakwambia Mungu akinipa uhai na majaliwa, nakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Manara

Simba SC kurejea mazoezini juma lijalo
Young Africans waanza kujiandaa kisaikolojia