Msemaji wa klabu ya Simba SC, Haji Manara amewatahadharisha wachezaji kuitambua thamani ya jezi ya klabu wanayochezea huku akidai kama haya yatatokea tena mkoani Kigoma (Julai 25), basi ataacha kazi ya usemaji.

Kama kawaida yake Manara ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufikisha tahadhari hiyo kwa wachezaji wote wa Simba SC.

Manara amemtumia Nahodha na Mshambuliaji wa kikosi cha Simba SC John Bocco kufikisha ujumbe kwa wanzake.

Ameandika: “Captain @john_22_bocco sema na wenzio bro,,,mtakuja kuua watu Kwa makundi siku moja ,naambiwa Dar kuna Shabiki kajipiga kitanzi huko,,,half ya kwanza mmecheza kama mmelazimishwa au mnadai kitu, mmezinduka second half na wao wakaweka contena mechi ikaisha,,,, Wallah Kigoma tukifungwa naacha hii kazi narudi Shamba kulima,,,,

Viongozi wanatimiza majukumu yao, Washabiki wanajaa kuliko Washabiki wao kwa mbali mno,, Mm natukanwa kutwa Kwa kuwapa nguvu nyie lakini mmeenda kutuangusha,,,,

Sioni sababu ya kuendelea na kazi hii kama wachezaji hawajui nn maana ya uzito wa Derby,,, Wachezaji wao wanajitoa asilimia elfu moja toka dakika ya kwanza,,,cc tunazinduka kushakuchwa,,,,

Kaeni wenyew zungumzeni na thamani ya jezi ya @simbasctanzania ilindwe.”

Simba SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans juzi Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Ujenzi wa sanamu la Magufuli viwanja vya sabasaba
Mgunda: Tutapiga panapouma