Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara pamoja na watu wengine 18 waliokuwa wanashikiliwa kuhusiana na sakata la kutekwa kwa Mo Dewji.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa wamewaachia kwa dhamana watu hao 19 leo kati ya watu 26 waliokuwa wanashikiliwa na jeshi hilo.
Aidha, Kamanda Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linaendelea kuwashikilia watu wengine saba kuhusiana na tukio hilo huku upelelezi ukiendelea.
Manara alikamatwa Oktoba 12 mwaka huu, kwa tuhuma za kutoa taarifa ambazo alidai kuwa zinatokana na familia ya Mo Dewji, madai ambayo jeshi la polisi lilisema sio ya kweli.
-
Afisa usalama wa taifa Kenya akamatwa na ‘unga’
- Walinzi waeleza kwanini hawakuwa na bunduki wakati Mo Dewji anatekwa
Msako wa watekaji wa Mo unaendelea katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam, tangu Oktoba 11 alipotekwa bilionea huyo katika hoteli ya Colosseum alipoenda kufanya mazoezi alfajiri.