Mkuu wa Idaya ya Habari na Mawasilino Simba SC Haji Sunday Ramadhan Manara amewajibu baadhi ya wadau wa soka nchini ambao wamekua wakimtabia mabaya kuhusu kazi wake ndani ya klabu hiyo.
Manara ametuma majibu hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, kufuatia madai yalitolewa na baadhi ya wadau hao wakisema amesimamisha kazi, huku akitakiwa kutozungumza lolote kuhusu Simba SC.
Manara ameandika kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii kuwa, bado yupo Simba SC, na ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida, huku akiwatuliza mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Amedai kuwa, huenda ukubwa na umaarufu wa jina lake unamponza hadi kufikai hatua ya kuzushiwa mambo kama hayo, lakini anahisi huenda hatua ya kuzushiwa majanga inatokana na kazi yake kuwavutia wengi ndani na nje ya nchi.
“Huu ukubwa wa jina langu unaniponza, umaarufu wangu unawaumiza wengine.
“Sikuwahi kutaka kuwa hivi, lakini kazi yangu naamini imewavutia wengi na Mungu akaamua kunipandisha.”
“Please Please Please (Tafadhali) Wanasimba mimi Haji wenu bado nipo nanyi na nitaendelea kuwa msemaji wenu hadi pale riziki yangu itakapokwisha, ( Hatatokea mmoja wetu kubaki milele iwe kwa kifo au vinginevyo ).
“Waambieni wenye kuandika tetesi za kuondoka kwangu, mimi mtu dhaifu lakini ni mjuzi mno katika mambo ya mawasiliano ya umma na nina uzoefu mkubwa katika eneo hili na nishakuwa sugu na changamoto za kazi.”
“Halafu waulizeni Simba namuachia nani ?
Haji aliwahi kutoa ufafanuzi kwa nini amekua kimya kwa majuma kadhaa, akisema uongozi wa Simba SC ulimpa mapumziko (Likizo) baada ya kufunga ndoa na mke wake Naheeda Abdallah, Desemba 10 mwaka huu 2020.