Mkuu wa Idara ya Habari Simba SC Haji Manara amekanusha kusambaza sauti yake kwenye mitandao ya kijamii, inayothibitisha uwepo wa tofauti kati yake na Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.
Manara amesema sio yeye aliyefanya hivyo na huenda Barbara amefanya kwa makusudi ili kuendelea kumuharibia ndani ya klabu hiyo, yenye historia kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Manara ameandika kwenye kurasa za Mitandao ya Kijamii kuwa: Jana nilisema sitaongea tena kuhusu hili jambo hadi game ipite na mamia ya watu wamenirai hivyo pia.
Lakini Kwa sababu anazozijua yy usiku wa jana akaamua kuvujisha clip niliyomtumia yy WhatsApp!!
Wengine wanadhani mm ndio nimeituma hyo clip,Sina muda na hivyo vitu ,,lau ningetaka kuachia lolote jana ,basi ningeachia mambo ya aibu na tuhuma zake zilizojaa vitisho kwangu.
Ninajua amefanya hivi kusudi ili atengeneze mazingira ya uovu kwangu ili likitokea la kutokea Kigoma aseme sababu ni Haji.
Narudia tena na tena sitaki kwa sasa kuongea lolote hadi mechi hii ipite, nisilazimishwe kusema sasa.
Yoyote anaedhani vinginevyo asubiri Jumatatu kisha tutoe hukumu.
Sitachafuka na ukweli utaniacha huru na mtajua kila kitu.