Msemaji wa klabu ya Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amesema klabu hiyo haitoi malalamiko kwa Waamuzi kwa makusudi ila inafanya hivyo kuwakumbusha wajibu wao wanapokua uwanjani.

Manara ametoa ufafanuzio huo, baada ya Hassan Bumbuli kuanika wazi namna ambavyo klabu ya Young Africans inavyoumizwa na baadhi ya waamuzi waliochezesha michezo yao hadi sasa.


Manara amesema: “Wajibu wetu ni Kukumbusha tu, ila sio kupeleka malalamiko kwa Waamuzi kwa kuwa sisi tuna mashabiki na wanaona kuwa Haki Haitendeki na wao kazi yao ni kusema kwa kuwa ndio kazi ambayo wameichagua.”

Mwishoni mwa juma lililopita Young Africans ilipata wakati mgumu dhidi ya Mbeya City FC kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana, huku madai ya baadhi ya wanachama na mashabiki wao wakisisitiza mwamuzi aliinyonga timu yao kwa shambulio na Mayele kuzimwa kwa kigezo cha kuotea.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania ikiwa na alama 36, ikifuatiwa na Mabingwa watetezi Simba SC yenye alama 31.

UEFA yaiwekea ngumu FIFA
Dola Milioni 127.2 kununua mabehewa