Klabu ya Manchester City imeweka rekodi ya mapato ya Premier League kufikia Pauni 712.8m kwa mwaka wa fedha wa 2022-23.
Hii inazidi rekodi ya Pauni 648.4m iliyowekwa mwezi uliopita na Manchester United na ni ongezeko la Pauni 99.8m ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Faida ya City ya Pauni 80.4m imepanda kutoka rekodi ya mwaka jana ya klabu hiyo iliyokuwa Pauni 41.7m.
Takwimu hizo zimekuja baada ya msimu uliopita kushinda mataji matatu na kuwa timu ya pili England kufanya hivyo baada ya Manchester United mwaka 1999 ilipotwaa Premier, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Baada ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kukamilika kwa ‘treble’ swali ambalo nilikuwa nikiulizwa mara nyingi, lilikuwa ‘Je, unaongozaje hapo?”
“Mafanikio ya leo yanamaanisha uwekezaji zaidi kwa kesho. Pia mafanikio yetu ya pamoja yananipa imani kubwa kwamba kwa pamoja tunaweza kutimiza hata zaidi katika miaka ijayo,” alisema Mwenyekiti wa Man City, Khaldoon al-Mubarak.
Taarifa ya fedha ya klabu inaonesha kuongezeka kwa vyanzo vyote vikuu vya mapato. Mapato ya matangazo yaliongezeka 20.2% hadi Pauni 299.4m.
City wanasema hiyo ilitokana na mafanikio yao katika Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA.
Klabu hiyo ilipata faida ya Pauni milioni 121.7 kwenye biashara ya wachezaji katika mwaka wa fedha wa 2022-23 na inasema jumla ya uhamisho uliofanywa baada ya Juni 30, 2023, ambao ulijumuisha kuwasili kwa Jeremy Doku, Mateo Kovacic, Josko Gvardiol na Matheus Nunes, pamoja na kuondoka kwa Cole Palmer, Riyad Mahrez, Aymeric Laporte na James Trafford.