Mabingwa wa soka nchini England Manchester City, wameweka masharti ya kumuachia mshambuliaji wao Leroy Sane, anaeripotiwa kuwa kwenye mipango mizuri ya kujiunga na FC Bayern Munich ya Ujerumani.

Manchester City wameitaka klabu hiyo ya mjini Munich, kumtoa beki wao wa kushoto David Alaba, ili awe sehemu ya uhamisho wa Sane.

Mkataba wa Sane na Manchester City utafikia tamati mwaka 2021, na nyota huyo bado hajaanza mazungumzo na klabu hiyo katika swala zima la kusaini mkataba mpya, huku taarifa zikieleza mshambuliaji huyo   anatamani kuondoka mjini Manchester.

Wachezaji wengi wa Kijerumani, waamini kucheza FC Bayern Munich, ndio njia rahisi ya kupata nafasi kwenye timu ya taifa ya Ujerumani.

Taarifa kutoka Ujerumani zinaeleza kuwa mkataba wa Alaba utafikia tamati mwaka 2021, na uongozi wa FC Bayern Munich upo tayari kumuuza kama atataka kuondoka kuanzia mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa zingine zinaeleza kuwa Manchester City, walikuwa wanahitaji kumsajili beki wa kushoto kati ya Lucas Digne na Ben Chilwell, hivyo dili hilo huenda likafa kama watafanikiwa kumsajili David Alaba wa Bayern Munich.

Alaba ni moja ya mabeki bora wa pembeni, wenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani.

WHO: virusi vya corona vinaweza visiishe kama ilivyo UKIMWI
TP Mazembe mabingwa DR Congo