Manchester City imeibuka na ushindi mnono baada ya kuwashushia kipigo kikali majogoo wa Liverpool kwa kuwachapa mabao 5-0.

Sergio Aguero alikuwa wa kwanza kuipatia Man City bao la kuongoza katika dakika ya 24 kabla ya Liverpool kuwa pungufu pale ambapo Sadio Mane kuonyeshwa kadi nyekundu.

Liverpool wakicheza pungufu walionekana kuzidiwa nguvu na Man City na kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza mshambuliaji raia wa Brazil Gabriel Jesus alipachika bao la pili na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini Man City ndio waliong’aa zaidi baada ya Gabriel Jesus kufunga bao la tatu dakika ya 53 kabla ya Leroy Sane kuimaliza Liverpool kwa kupiga mabao mawili dakiza za lala salama na kufanya Man City kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Sadio Mane alionyeshwa kadi nyekundu

Baada ya ushindi huo wa mabao 5-0 Manchester City wamefikisha pointi 10 wakiwa tayari wamecheza michezo minne

 

 

Mahita aunguruma, ampa neno IGP Sirro
Jaji Lubuva akerwa na kauli za wanasiasa