Imeripotiwa kuwa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City hawakutuma ofa kwa ajili ya kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham, kama taarifa zilivyozagaa mtandaoni.

Imefahamika ya kwamba Bellingham mwenye umri wa miaka 19, tayari ameonesha nia ya kujiunga na Real Madrid baada ya taarifa kuibuka timu hiyo imekubali maslahi binafsi na Borussia Dortmund huku Man City ikihusishwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Ühamisho wa Belligham unatarajiwa kufanyika katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwisho wa msimu huu, lakini kwa upande wa Man City imejiweka kando kwanza.

Hatma ya Bellingham kwenye klabu ya Borussia Dortmund imekuwa gumzo kubwa akihusishwa na timu kibao kama Mančhester United, Liverpool, Paris Saint-Germain na FC Bayern Munich.

Kwa mujibu wa gazetí la Athletic, ni wazi Man City imekubali kwamba Bellingham anataka kujiunga na Los Blancos, lakini hawajatuma ofa licha ya Pep Guardiola kuvutiwa na kiungo hiyo. Thamani ya Bellingham inaaminika ni zaidi ya Pauni 100.

Akizungumzia kuhusu tetesi za Bellingham wakala wake Edin Terzic alisisitiza hana taarifa yoyote mpaka sasa.

“Sijasikia chochote kutoka kwake kama anabusishwa na timu, ingawa aliwahi kuzungumza kuhusu hatima yake akisisitiza Dortmund ndio sehemu pekee ya kuendeleza kipaji chake.”

Robertinho kuibomoa Vipers SC
Dube achekelea kuzifunga Simba, Young Africans