Mchezo wa ufunguzi wa pazia la ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu ujao wa 2019-20, kikosi cha Manchester United kitakuwa na kibarua kigumu cha kuvaana na Chelsea ambapo mtanange huo utapigwa kwenye dimba la Old Trafford mnamo Agosti 11.
Imeripotiwa kwamba msimu wa kwanza mahususi wa Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa United utaanza kwa mchezo huo unao tarajiwa kuwa mgumu pande zote, Chelsea itashuka dimbani bila ya Eden Hazard ambayo imemaliza msimu kwa kunyakua taji la UEROPA na kubaki kwenye nne bora ya msimamo wa ligi ya Uingereza.
Hivi karibuni Manchester imekua na wakati mgumu kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu waliyokuwa wakiyapata, ambapo wamemaliza msimu uliopita bila ya taji lolote na kukosa nafasi ya kushirki nafasi ya kuwepo kwenye michuano ya UEFA kwa msimu ujao.
Kwa upande mwingine Tottenham Hotspurs pia itakuwa na mtanange mgumu mwanzoni mwa msimu huo ambapo spurs watamenyana na Manchester City na Arsenal ugenini kwenye mechi zao nne za mwanzo.