Wakati mlinda mlango namba moja wa Manchester United mhispania David De Gea akihusishwa kuihama timu hiyo hali imekuwa tofauti kwa upande wake hadi katika uongozi wa mashetani hao wekundu ambao wameonekana wakigoma kumuongeza mshahara kipa huyo.
Taarifa kutoka kwenye timu hiyo zinasema mabosi wa De Gea wamevunja ukimya na kwa kusimamia misimamo yao ambapo wamenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa wapo tayari kumpa mshahara wa £ 350,000 na si vinginevyo.
Mabosi hao wa United wamemuambia kipa huyo kwamba hawatomuongeza pesa zaidi ya hapo ambayo watakua wakimlipa kwa wiki kama ilivyo kawaida ya ulipaji wa mishahara ya wanasoka wengi barani ulaya na endapo kama ataamua kuikacha timu hiyo kwa kigezo cha ufinyu wa mshahara basi milango ipo wazi na anaweza kuondoka.
Licha ya kipa huyo kusemwa vibaya kutokana na kiwango chake kuporomoka ambapo katika msimu uliopita na kufungwa magoli mengi ya kawaida na kushindwa kuisaidia timu yake kunyakua taji lolote na kukosa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani ulaya lakini baadhi ya vilabu katika bara hilo vimeonekana kumuhitaji vikiwemo Paris Sant German ya Ufaransa na Bayern Munichen ya Ujerumani.