Beki kutoka nchini Ivory Coast, Eric Bailly amefanyiwa vipimo vya afya na klabu ya Manchester United ikiwa ni sehemu ya mpango wa kusajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 30, akitokea Villarreal ya nchini Hispania.

Klabu hizo zimeshakubaliana dau la mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 na aliwasili mjini Manchester kukamilisha uhamisho wake na wawakilishi wake wanatarajiwa kuwa wamemaliza dili hilo hadi kufikia Ijumaa.

Bailly ambaye ni miongoni mwa mabeki bora Hispania kwa sasa, atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya, Mreno Jose Mourinho Manchester.

Villarreal wapo tayari kuwauzia Man Utd, mchezaji huyo waliomnunua kutoka kwa wapinzani wa La Liga, Espanyol Janaury 2015 kwa matarajio ya kupata faida ya Pauni Milioni 4.4.

Mbali na Bailly, anayewaniwa na Bayern Munich, Barcelona, Paris Saint-Germain, Arsenal na Manchester City, Mourinho pia anataka kuimarisha kikosi Man United kuwa kuwasajili Zlatan Ibrahimovic aliyemaliza Mkataba PSG na Nemanja Matic wa Chelsea.

Bajeti ya Kwanza ya Magufuli kusomwa leo, Ukawa waahidi kutoa vipande na kususa
Stephen Okechukwu Keshi Amefariki Dunia