Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw jana aliondolewa kwenye kikosi cha England kitakachoivaa Slovakia leo usiku.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa ni Manchester United ambao wameomba mchezaji huyo apumzishwe, ikiwa ni kama tahadhari ya kuepeuka nyota huyo kupata majeraha.
Zaidi ya hapo kwa mujibu wa Tweet kutoka klabu ya Manchester United mchezaji huyo atarejea kufanya mazoezi na wenzake badala ya kuendelea na kambi ya timu ya taifa.

Ratiba Ya Leo Michezo Kufuzu AFCON 2017
Mesut Ozil Aitaka Jezi Namba 10 Atamani Kuwa Zinedine Zidane