Klabu ya Soka ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United katika mchezo huo ambao umeacha rekodi mbalimbali yamefungwa na Paul Pogba dakika ya 3 kwa penati na Luke Shaw dakika ya 83 huku Jamie Vardy akifunga la Leicester City dakika ya 90+2.
Katika mchezo huo umewafanya Man United kutopoteza mechi hata moja kati ya 122 za EPL kwenye uwanja wa Old Trafford pale ambapo walianza kutangulia kufunga, mara ya mwisho kutangulia kufunga kisha wakapoteza ilikuwa ni mwaka 2009 ambapo walipoteza 4-1 dhidi ya Liverpool.
Aidha, kocha Jose Mourinho ameweka rekodi ya kutopoteza mechi katika michezo yake 18 ya ufunguzi wa ligi katika maisha yake ya ukocha. ambapo ameshinda mechi 9 kati ya 10 za ufunguzi kwenye EPL pekee ambako pia ametoa sare 1, huku mfungaji wa bao la pili la timu hiyo, Luke Shaw amefunga bao lake la kwanza ndani ya United ikiwa imemchukua mechi 67 katika mashindano yote.
Kwa upande wao Leicester City wameweka rekodi mbovu ya kuwa timu ya kwanza kufungwa bao la kwanza la msimu kwenye ligi kuu ya Uingereza ndani ya misimu mitatu mfululizo ya hivi karibuni.
-
Hofu ya 2018/19 yamvuruga Mourinho, asema na uongozi
-
Ricardo Rodriguez kuziba pengo Arsenal
-
Niko Kovac ampinga bosi wake FC Bayern Munich
Hata hivyo, hii imekuwa ni mara ya pili katika historia ya ligi kuu ya Uingereza mechi ya ufunguzi kuchezwa Ijumaa na mechi zote Leicester City imecheza na kupoteza. mara ya kwanza ilikuwa msimu uliopita ambapo ilikubali kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Arsenal
,