Klabu ya Manchester United inadaiwa kumevutiwa na beki wa kulia wa Galatasaray ya Uturuki, Sacha Boey.
Boey anafuatiliwa na klabu nyingi za ligi Kuu England zikiwemo Arsenal, Brighton na Burnley.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejihakikishia namba ya kudumu Galatasaray katika kipindi kirefu na amepata uzoefu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Kwa mujibu wa SporX.com wachapishaji wa habari za michezo kutoka Uturuki, Klabu ya Man United inamtolea macho beki huyo.
Taarifa zinadai kuna ongezeko kubwa la timu kutoka England zikimtamani Boey, ambaye mkataba wake utafikia kikomo mwaka 2025.
Boey alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Rennes mwaka wa 2019 na akahamia lstanbul mwaka 2021 kabla ya kujunga kwa mkopo Dijon inayoshiriki Ligue 1.
Ingawa ameiwakilisha Timu ya Taifa ya Vijana ya Ufaransa, pia alijumuishwa katika kikosi cha Cameroon hapo awali.