Wakati kikosi chao kikiendelea na maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya, ambapo usiku wa kuamkia Alhamisi waliambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Real Madrid, inaelezwa mabosi wa Manchester United wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa straika wa Atalanta, Rasmus Hojlund.
Maandalizi ya Manchester United ya kabla ya msimu mpya yanaendelea huku Erik ten Hag akipania kukiimarisha kikosi chake kabla ya kampeni mpya ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Mashetani hao wekundu walichapwa 2-0 na Real Madrid usiku wa kuamkia Alhamisi na sasa wanatazamia mpambano mwingine wa kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund kesho Jumatatu (Julai 31).
Ten Hag ana Imani kwamba Mashetani wekundu watafanikisha mpango wa huyo wa kimataifa wa Denmark, lakini mchezaji huyo anaonekana kutaka kubadili.
United hadi sasa hawajafikia thamani ya Pauni Milioni 80 ya klabu hiyo ya Italia.
Mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili yameanza, huku timu hiyo ya Ligi Kuu ikiwa na matumaini ya kufikia makubaliano kwa wakati ili kuanza kumtumia Hojlund watakapoanza kampeni yao ya EPL Agosti 14, mwaka huu dhidi ya Wolves.