Ligi kuu Uingereza inaendelea usiku wa leo raundi ya 14 kwa mechi 6 zitakazopigwa kuanzia majira ya ya 10:30 usiku. Michezohiyo yenye msisimko wa hali ya juu itawakutanisha vigogo mbalimbali wakiwemo Manchester United,Arsenal,Manchester City na Arsenal.
Arsenal vs Manchester United
Mchezo unaotazamwa zaidi ni Manchester United dhidi ya Arsenal utakaopigwa dimba la Emirates majira ya 11:15. Huu ni mchezo muhimu kwa pande zote kwani kama Arsenal wataibuka na ushindi basi watafikisha alama 28 na kuendelea kusalia nafasi ya pili nyuma ya Liverpool wenye alama 34. Endapo United ataibuka na ushindi katika mchezo huo atafikisha alama 22 na kupanda mpaka nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi.
Nottingham vs Manchester City
Manchester City wamepoteza michezo mitano mfululizo ya mashindano mbalimbali wanayoshiriki.Kwa sasa wanashika nafasi ya 5 wakiwa na alama 23,kama wataibuka na ushindi katika mchezo huo watafikisha alama 26 na kurejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na hiyo itawarudisha kwenye hali ya kutetea ubingwa. Kwa upande wa Nottingham Forest wao wanashika nafasi ya 6 na kama wataibuka na ushindi kwenye mchezo huo watafikisha alama 25 na kupanda mpaka nafasi ya 4 inayokaliwa na Brighton kwa sasa
Newcastle United vs Liverpool
Michezo 5 ya mwisho kwa Liverpool wamefanikiwa kukusanya alama 13 wakishinda mechi 4 na sare 1 wapo kileleni kwa alama 34 wakiwazidi Arsenal kwa alama 9.Usiku wa leo Arne Slot ameapa kwenda StJames Park kuendeleza rekodi nzuri aliyoandika kwa msimu huu akiwa na washambuliaji wake tegemezi ambao ni Darwin Nunez,Salah na Gakpo.
Newcastle United hawajaanza vyema msimu huu baada ya kuvuna alama 19 katika michezo 13 waliyocheza.Kama wataibuka na ushindi basi watafikisha alama 22 na hiyo itawarudisha kwenye mbio za ubingwa kwa msimu huu.
Southhampton vs Chelsea
Chelsea wako katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 25 sawa na Arsenal ,Kama wataibuka na ushindi dhidi ya Southampton watafikisha alama 28 na kukaa nafasi ya pili katika harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza. Chelsea chini ya kocha Maresca imefanya vyema kwenye michezo 5 iliyopita wakishinda michezo mitatu na sare 2.