Ligi kuu ya Uingereza imeendelea wikiendi hii kwa michezo mbalimbali. Manchester United imeendelea kufanya vibaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Brighton katika dimba la Old Trafford. Kipigo hicho kinawafanya United kuteremka mpaka nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 26.
Ikumbukwe United imeshinda mchezo mmoja tu kati ya saba iliyocheza na Brighton siku za hivi karibuni. Kwa upande wa Everton mambo yameanza kuwa mazuri baada ya kuwasili kwa Kocha David Moyes. Ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tottenham unaifanya klabu hiyo ya Mersey Side kurejesha matumaini kwa mashabiki wake baada ya kufikisha alama 20 katika mechi 21 walizocheza hivi karibuni.
Nottingham Forest wameendelea kufanya vyema kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton.Ushindi huo unawafanya Nottingham kufikisha alama 44 na kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.Forrest wana alama na Arsenal na wametofautiana alama 6 pekee na Liverpoo vinara wa ligi kuu.
Mancity yarejea nne bora
Ushindi mnene wa mabao 6-0 dhidi ya Ipswich United umerudisha matumaini ya klabu hiyo kuwania nafasi nne za juu. Katika mchezo huo City walipata bao la uongozi dakika ya 27 likiwekwa kimiani na Phil Foden,Bao la pili liliwekwa kimiani na