Klabu ya Southampton imemsajili mlanda mlango kutoka nchini England Alex Simon McCarthy kwa mkataba wa miaka mitatu.

McCarthy amejiunga na klabu hiyo ya St Mary’s Stadium, akitokea Crystal Palace.

McCarthy ambaye alicheza michezo saba akiwa na Crystal Palace msimu uliopita, amefanikisha safari ya kuondoka jijini London kutokana na msukumo mkubwa uliotolewa na meneja mpya wa klabu ya Southampton, Claude Puel.

Jukumu kubwa kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 26 baada ya kusajiliwa klabuni hapo, litakua ni kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Fraser Forster ambaye anaendelea kujiunguza.

Steve Mandanda

Hata hivyo kuondoka kwa McCarthy huko Selhurst Park, kumemuepusha na changamoto kubwa ambayo alitarajia kukutana nayo, kufuatia hatua ya kusajiliwa kwa mlinda mlango kutoka nchini Ufaransa Steve Mandanda pamoja na Wayne Hennessey wa Wales.

Video: Mrema kufikisha Majina ya Polisi Wanaolazimisha Rushwa kwa Magufuli
Alex Song Atimkia Urusi