Mshambuliaji wa klabu ya Mwadui FC, Rashid Mandawa yupo nchini Vietnam akifanya majaribio ya majuma mawili  katika Klabu ya Dongtam An Long FC inayoshiriki Ligi Kuu Vietnam .

Mandawa maarufu kama Chidikidebe amesema kuwa awali hali ya hewa ya nchini humo ilikuwa ikimsumbua lakini kwa sasa ameweza kuzoea hali hiyo.

“Mambo yanaenda vizuri na ninakaribia kurudi nchini Tanzania tatizo lililonikabili mwanzo ni hali ya hewa ila sasa nimezoea,” alisema Mandawa

Endapo Mandawa atafanikiwa kwenye majaribio hayo atakuwa mchezaji wa tatu akiwemo Nizar Khalfan na Danny Mrwanda ambao waliwahi kuichezea Al Tadoon ya nchini humo.

Soka La Bongo Lamuweka Jamal Malinzi Katika Mtihani Mzito
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo atimuliwa, mamilioni yapotea hovyo