Bondia wa ngumi za kulipwa, Karim Mandonga, anatarajiwa kufanyiwa kipimo cha kichwa baada ya kupata jeraha kutokana na kipigo alichopokea Julai 29, mwaka huu jijini Mwanza.
Mandonga alipigwa kwa TKO na Moses Golola wa Uganda katika pambano la raundi nane lisilo la ubingwa la uzito wa juu.
Kutoka na kipigo hicho, Mandonda aliumia kichwa na kuifanya Kamisheni ya Ngumi ya Kulipwa Tanzania (TPBRC, kutangaza kumsaidia kupata vipimo kisha matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
Mandonga mwenye umri wa miaka 42 alipigwa kipigo hiko na bondia, Moses Golola kutoka Uganda katika pambano la raundi nane lisilo la ubingwa uzito wa juu.
Katibu wa TPBRC, George Lukindo amesema kuwa, pamoja na kupelekwa kupata vipimo, Mandonga hataruhusiwa kucheza pambano lolote kwa kipindi cha miezi sita.
Amesema Shirikisho litasimamia uchunguzi wa afya ya bondia huyo na kumsimamia kwa karibu kwa mujibu wa kanuni ya mchezo wa masumbwi baada ya bondia kupigwa kwa TKO au KO.
Kocha wa Mandonga, Said Kisopu, amethibisha kupokea barua ya TPBRC ya bondia wake kutakiwa kwenda kufanya vipimo vya afya chini ya Shirikisho.
Kisopu amesema pamoja na Shirikisho kusimamia vipimo vya bondia wake, uongozi utahakikisha Mandonga anapata matibabu ya kina na kurudi ulingoni baada ya miezi sita.