Wakati mchezo wa fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ukitarajiwa kupigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa NSC Olimpiyskiy mjini Kiev nchini Ukraine, mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane ametuma jezi 300 za Liverpool katika kijiji alichozaliwa nchini Senegal.
Kesho itakuwa ni siku kuu ya kipekee katika kijiji hicho ambapo watu wanatarajia kukusanyika kwa pamoja kufuatilia mchezo huo wa fainali kwenye runinga wakiwa wamevalia jezi nyekundu za klabu ya Liverpool.
Mane amesema kuna watu zaidi ya 2000 katika kijiji hicho na kesho hawata fanya kazi yoyote. ”Familia yangu bado ipo kijijini, Mama yangu na mjomba wangu. Nimenunua jezi 300 nakuwatumia watu kijijini wazivae wakati wakiangalia mchezo wa fainali”, alisema Mane.
-
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Ufaransa
-
Rais wa Ghana amsweka ndani Mwenyekiti wa Shirikisho la Kandanda
Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa watu kijijini kwao ‘Bambali’ wamefurahi hasa rafiki yake anayeitwa Youssouph Diatta ambaye wamekuwa pamoja tangu wakiwa shuleni na walitazama wote mchezo wa fainali ya kusisimua mwaka 2005 kati ya Liverpoo na AC Milan wakiwa na miaka 14 ambapo Liverpool waliibuka mabingwa.