Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani, Ramadhan Maneno amesema kuwa atahakikisha anakomboa maeneo mbalimbali yanayoongozwa na vyama vya upinzani mkoani humo katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

Amewataka wanachama chama hicho kuachana na siasa za mazoea ambazo zimekuwa zikikiumiza chama hasa nyakati za uchaguzi ambapo husababisha wanachama kuwapigia kura wapinzani na kukikandamiza chama.

Ameyasema hayo Chalinze wakati wa sherehe za kumpongeza kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo zilizoandaliwa na CCM kata ya Bwilingu.

 

“Kuna kata, vitongoji, Vijiji na mitaa vinashikiliwa na upinzani ambapo waliongoza wakati wa chaguzi zilizopita ni lazima tuzirudishe,“amesema Maneno

 

Hata hivyo, ameongeza kuwa siasa za mazoea zimekiharibu chama kwa watu kushindwa kuwakemea wale wanaokwenda kinyume na katiba ya chama na kujiona kuwa wao ni miungu watu.

BoT yaimwagia mabilioni Serikali
Msigwa awapongeza Askofu Kakobe na Gwajima