Zimbabwe, manesi 15,000 wamesimamishwa kazi kufuatia mgomo uliokuwa unaendelea nchini humo wa manesi hao kutaka kupandishiwa mshahara richa ya kuwa tayari Serikali ya nchi hiyo imekwishatenga kiasi cha Dola 17,114,446 sawa na Bilioni 39 kwa pesa ya kitanzania.

Makamu wa Rais nchini humo, Constantino Chiwenga amesema Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukerwa na manesi hao waliogoma kusitisha mgomo wao hata mara baada ya Serikali  kuwawekea fedha hizo katika akaunti ya Wizara ya Afya ili kushughulikia malalamiko yao.

”Serikali imeamua kufanya hivyo kwa manufaa ya wagonjwa na kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa, kuwafukuza kazi manesi wote wanaofanya mgomo na kusababisha madhara katika nchi” amesema Chiwenga.

Ambapo manesi hao waligoma kusitisha mgomo huo wakidai kuwa hawaridhishwi na kiasi cha fedha kilichoweka kwa ajili ya kuongeza mishahara yao wakidai kuwa badi ni kidogo.

Serikali imesema kukataa kwa fedha hizo na muendelezo wa mgomo huo kunaashiria msukumo wa kisiasa na si kuhusu maslahi kama wanavyodai wao.

Kwa sasa Serikali imeazimia kuajiri manesi wapya na kuwarudisha wale waliostaafu ili kushughulikia upungufu huo uliojitokeza.

Kufuatia mgomo huo uliofanywa na manesi wagonjwa mbalimbali wamelazimishwa kurudishwa nyumbani kupisha mgomo huo.

 

Mwalimu wa Chuo asitishwa kazi kwa kumtaka kimapenzi mwanafunzi
Polepole ajibu wanaotuhumu ripoti ya CAG, ataka wachukuliwe hatua