Mwanaharakati wa mitandao ya kijamii, Mange Kimambi amepatwa na hofu kubwa baaada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, Robert Boaz, kufunguka na kusema hawatomvumilia yeye pamoja na kundi lake kwa vitendo wanavyofanya vya kuwakejeri na kuwatukana viongozi wa nchi.

Mange baada ya kupata taarifa hizo kutoka katika gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha hofu hiyo ameandika haya;

”Ila hawa watu siku wakinikamata mimi jamani ntajuta, kwanza nahisi Magu atanitatua marinda yooote ndo atanikabidhi kwa Bashite nipigwe shoti za chuchu” amesema Mange Kimambi.

Hata hivyo Boaz amesesma watu wanaoshirikiana na mwanaharakati huyo kutoa taarifa za uongo, uzushi, matusi, na kejeli watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi.

’Tunafanya uchunguzi Mange hatutamuacha, kuna wengi wanaonunua kesi wataenda mahakamani kwa kushirikiana kutoa taarifa za uongo, hatutakubali kutumiwa vibaya kwa mitandao na kufanya kejeli na dharau kwa viongozi’’

Bahati mbaya nasikitika kwamba kuna baadhi ya watu wale mambao tunapata taarifa zao tutawapeleka mahakamni, pale ambapo tutathibitisha kwamba wameshiriki ku-upload (kupandisha), taarifa za uongo, matusi , kejeli.

Liverpool wapinga kadi nyekundu ya Sadio Mane
Video: Makonda azidi kuiboresha Dar, biashara ya magari kufanyika Kigamboni tu