Ndani ya Chama cha Mapinduzi – CCM, jina la Philip Mangula limejipatia umaarufu mkubwa na kupelekea Kiongozi huyu mstaafu kuitwa ‘mzee wa mafaili’ huku baadhi ya watu wakihoji sababu ya jina hilo na maana yake.

Ili kupata majibu sahihi ya kuujulisha umma na kuepuka upotoshaji ama kupotoshwa, Dar24 Media imemtafuta Mzee Mangula ambaye ametolea ufafanuzi wa jina hilo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake hivi karibuni jijini Dodoma.

Philip Japhet Mangula ni mmoja wa makatibu wakuu wanne wa CCM, waliotolewa kwenye nafasi za ukuu wa Mkoa na kupelekwa kushika nafasi ya juu ya utendaji ndani ya chama, akiwa na historia ya kusimamia chaguzi kuu mara mbili mfululizo na mara zote CCM ilishinda.

Philip Japhet Mangula. Picha na Dar24 Studio.

Anasema, aliwahi kuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Chama ambayo kimsingi ndiyo chombo cha kuangalia mwenendo wa kila mgombea, kwa ngazi zote za chama kama anafaa kupewa nafasi ya uongozi.

“Sasas katika nafasi hii kila mwana-CCM anapotangaza kugombea, kamati anatengenezea faili kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wake kimaadili, sasa nadhani hapa ndiyo lilitokea hilo jina na huwa nalisikia hata kwa wakubwa zangu, Mzee wa Mafaili nacheka halafu basi,” anafafanua Mzee Mangula.

Katika nafasi yake kama Katibu Mkuu wa CCM, Mangula alisimamia uchaguzi mkuu mara mbili, uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ambao ulikuwa ni uchaguzi mkuu wa pili kufanyika nchini, katika mfumo wa vyama vingi vya siasa ulioanza mwaka 1992, ukiwa mgumu kwa CCM na wa kwanza ulifanyika baada ya kifo cha muasisi wa Taifa (Mwl. Julius Nyerere), cha Oktoba 14, 1999.

KMC FC yamuwinda Andrew Simchimba
Sadio Mane: Nitaendelea kucheza Bayern Munich