Mwenyekiti wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Murtanza Mangungu amesema mipango ya usajili wa Dirisha Dogo inakwenda vizuri na wamejipanga kufanya usajili kwa umakini mkubwa.

Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji wazawa na wale wakimataifa, ambao wataingizwa kwenye kikosi ili kuongeza nguvu.

Mangungu amesema Uongozi unafahamu Mashabiki na Wanachama wanataka kuona timu yao inaimarika kwa kuwa na kikosi imara, ambacho kitafanikisha mpango wa kutetea Ubingwa.

“Tunajua kwamba wengi wanataka kusikia tutafanya nini kwenye wakati huu wa usajili, hatuna presha na jambo lolote,tutafanya usajili wa maana na mzuri.”

“Kikubwa ni kuwa na subira unajua mambo mazuri hayahitaji haraka na kwa na kila kitu kinahitaji mikakati imara,” amesema Mangungu.

Dirisha Dogo la usajili limefunguliwa Desemba 15 na linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2022 ambapo kwa sasa timu zimeanza harakati za usajili.

Saido atamba Young Africans Bingwa 2021/22
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 21, 2021