Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu amekanusha kauli ya Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Ismail Aden Rage, ambaye alidai kiongozi huyo hana mamlaka zaidi ya kufungua na kufunga vikao na Mikutano ya wanachama.

Rage alitoa kauli hiyo siku chache baada ya Simba SC kutupwa nje ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa kufungwa na Young Africans 1-0, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mangungu amemjibu Rage akiwa katika Kipindi cha Sports HQ cha EFM Radio leo Ijumaa (Julai Mosi), ambapo amesema: “Mimi ni Mtu Mzima, namuheshimu sana Aden Rage kwa kuwa amekua rafiki yangu kwa muda mrefu sana kwa miaka mingi nimekua naonana nae na hata baadhi ya vitu tulishawahi kushirikishana kuhusu SIMBA”

“Kauli yake ya Kuhusu mimi ni Mwenyekiti wa KUFUNGUA NA KUFUNGA VIKAO TU, Niliisikia na nikaitafakari kwa kina sana kwa kuwa yeye hajui kwa undani mangapi mazuri ambayo tunayafanya ndani ya Bodi mpaka kuifikisha klabu hapa ilipo”

“Anaweza kuona mimi ni mwenyekiti wa Vikao, ila amesahau mafanikio ya klabu kwa misimu minne iliyopita Bodi ilikua ni hii hii na bado tunaendelea kuyafanya makubwa ndani ya klabu”

“Sisi sio watu wa Kubabaisha na hata hizo kauli ni za KIBAGUZI tena UBAGUZI wa Kimaendeleo kwa mambo mazuri na makubwa ambayo hawawezi kuyaona ukiwa nje ya klabu.”

https://www.youtube.com/watch?v=VYwodJIMI9o

TPLB yaanika mkeka wa Play Off
Mwenyekiti Simba SC amjibu Bernard Morrison