Manispaa ya Ilala iliyopo jijini Dar es salaam imekabidhi mkopo wa shilingi mil. 153,000,000 kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Zoezi la utoaji wa mikopo hiyo limeongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jumanne Shauri ambapo kila kikundi kilipewa Hundi ya shilingi millioni 3 na Kikundi cha Vijana kilichopo Kitunda kilipewa milioni kumi.
Amesema kuwa dhumuni la utoaji wa mikopo hiyo ni kuwawezesha wajasiriamali wa manispaa hiyo wawe na maisha ya Kati waweze kujishughulisha na Biashara na kujiingizia kipato chao.
“Serikali yetu tukufu inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano, Dkt. John Magufuli imetekeleza utoaji wa mikopo kwa awamu ya kwanza kwa vikundi mbalimbali ambapo Jumla ya shilingi 153,000,000 zimetolewa,”amesema Shauri.
Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Ilala, Fransisca Makoye amesema kuwa kigezo cha kwanza kwa mtu anayechukua mkopo lazima awe anatoka Manispaa ya Ilala ajulikane mtaa na kata anayotoka.
Aidha Makoye ametoa rai kwa vikundi vyote vilivyochukua mkopo kutumia fursa hiyo katika kujiendeleza na kuweka Mikakati yao ya Biashara na kujenga mtandao wao Wajasiriamali.
Hata hivyo, ameongeza kuwa mpaka kufikia Mwaka 2018 Manispaa ya Ilala imeshatoa kiasi cha shilingi 4,034,200,000 kwa wanufaika 15,388 kwa utaratibu wa awali.
-
Aliyesuluhisha ugomvi wa wanandoa auawa
-
Lugola aagiza mkurugenzi wa kampuni Arusha asukumwe ndani
-
Taasisi Binafsi Njombe zakwepa kutumia mashine za EFD