Kampuni ya Quality Group Limited imekubali kuachia eneo la wazi ililokuwa ikilipigania na Serikali kwa muda mrefu huku ikidai kuwa ni mali yake ambayo ilishinda mahakamani kihalali.
Aidha, eneo ambalo lililokuwa likigombewa na Kampuni hiyo ni lile la kuanzia mnara wa mataa(Light house mpaka bwalo la maafisa wa polisi(police officers Mess) barabara ya Toure jijini Dar es salaam.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Mkurugeenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Yusuph Mehbub Manji imesema kuwa imewaagiza mawakili kujitoa katika Rufaa iliyowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kutodai gharama yeyote iliyosababisha hasara za uendeshaji wa kesi hiyo.
“Ninaomba radhi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli na Serikali kwa sintofahamu iliyojitokeza wakati wa ufuatiliaji wa jambo hili, pia tunawaomba radhi wadau wote tuliowakwaza kisheria wakati wa ufuatiliaji kwa muda wa mwaka mmoja, tunasikitika sana kwa hilo, tunawaomba wananchi tumuunge mkono raisi wetu, kwani anadhamira ya kweli,” amesema Manji.
Hata hivyo, katika taarifa hiyo imesema kuwa Quality Group inatambua na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kizalendo na kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi.