Mwenyekiti wa Timu ya Yanga, Yusuph Mehbub Manji amejitokeza hadharani na kuthibitisha kuwa taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii inayohusu kujiuzuru kwake amesema kuwa ni ya kweli.
Mapema hii leo, taarifa hiyo ilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, kitu ambacho kilimfanya Katibu Mkuu wa Yanga kujitokeza na kukanusha taarifa hiyo na kusema siyo ya kweli hivyo kuwataka wanachama kupuuza taarifa hiyo.
Aidha, dakika chache baadaye, Yusuph Manji alisikika kupitia chombo cha habari (Efm) akikubari na kukiri kuwa taarifa hiyo ni ya kweli na imejieleza vizuri na kuongeza kuwa nafasi yake itakaimiwa na makamu mwenyekiti mpaka utakapofanyika uchaguzi.
“Nikweli taarifa hiyo ni ya kwangu kila mmoja aliyeisoma imejieleza vizuri na imeeleweka, Yanga ni yetu sote kwa hiyo mwanachama yeyote ana haki ya kuiongoza timu yetu,”amesema Manji.