Bingwa wa dunia wa masumbwi anayetajwa kuwa bondia bora wa muda wote, ameanza kumpika mwanaye Jimuel anayetaka kuingia rasmi ulingoni.

Jimuel mwenye umri wa miaka 18 ameanza rasmi mafunzo ya mchezo huo huku wazazi wake wakimsihi kuachana nao kutokana na namna ambavyo ni hatari kwa maisha ya wachezaji.

Pacquiao amelazimika kuanza kumpa mafunzo hayo baada ya Jimuel kusisitiza kuwa anaupenda mchezo huo kutoka ndani ya nafsi yake.

Mke wa Pacquiao, Jinkees ameeleza kuwa alitokwa machozi baada ya kusikia mwanaye ameamua kuingia kwenye mchezo wa masumbwi na hata kuanza kushiriki ngumi za ridhaa (armature), akishinda pambano lake la kwanza.

“Nilipokuwa nawaangalia, nilitokwa machozi. Mwanangu anataka kweli kuwa bondia. Nilimwambia mwanangu acha ni mchezo hatari, baba yako aliingia huko kwa sababu ya umasikini tu, lakini alisisitiza anataka kucheza kama baba yake,” Jinkees ameandika kwenye Instagram akiambatisha na picha ya Pacquiao akimfua Jimuel.

Pacquiao ambaye sasa ana umri wa miaka 40, hivi karibuni alishinda pambano lake la 70 dhidi ya bondia machachari kijana, Adrian Broner. Mwanaye anataka kuwa na uwezo wa kuiwakilisha nchi yake kama baba yake.

Rais Magufuli awapa ajira vijana 2000 wa JKT
LIVE VIDEO: Tafrija ya Kutoa Zawadi kwa Mshindi wa Wimbo Bora wa AFCON2019 U17

Comments

comments