Kiza kimetanda katika kambi ya bondia kutoka nchini Uingereza, Amir Khan, kufuatia kigugumizi kilichojitokeza kwa mpinznai wake Manny Pacquiao, ambaye anatararia kupambana nae mapema mwezi April mwaka 2016.

Khan, ameonyesha kuwa tayari kupanda ulingoni kumaliza ubishi na bondia huko kutoka nchini Ufilipino, lakini jana jioni muwakilishi wa Pacquiao, alitoa taarifa za kuutaka upande wa wanaoandaa mpambano huo kuwa na subira.

Sababu kubwa iliyotanjwa na muwakilishi wa Pacquiao, aitwaye Jeff Powell, imeonyesha kutokua na mashiko kutokana na bondia wake kuamini huenda kukawa na nafasi nyingine ya kupambana na Floyd Mayweather.

Kutokana na maelezo hayo, kambi ya Pacquiao imechukua tahadhari ya kuona kama atahitaji muda mrefu wa kujiandaa endapo Mayweather atabadili maamuzi ya kustaafu na kurejea ulingoni kukata ngebe za mpinzani wake.

Hata hivyo taratibu za pambano la Pacquiao dhidi ya Khan zilikuwa zimeshaanza kuchukua nafasi kubwa katika kila nyanja, lakini hatua iliopo sasa inadhihirisha huenda kuna baadhi ya mambo yakasimama kwa muda.

Ikumbukwe kuwa, Manny Pacquiao alishindwa kufua dafu mbele ka Floyd Mayweather katika mpambano wa May 02 mwaka huu, baada ya kushindwa kwa point.

DJ Mwenye Umri Wa Miaka Mitatu Ashinda Shindano La ‘SA Got Talent’
Infantino Adhihirisha Sarakasi Za Uchaguzi Wa FIFA