Manowari ya jeshi la Marekani ambayo ilizama wakati wa vita vya pili vya dunia, imepatikana kwenye bahari ya Pacific.

Ni miaka 72 sasa baada ya Manowari hiyo kuzamishwa na nyambizi wa Japan ambapo ilikuwa ikirejea kutoka oparesheni ya siri ya kupeleka sehemu za kuunda bomu la atomic ambalo baadaye lilitumiwa huko Hiroshima.

Meli hiyo ilipatikana kilomita 5.5 chini ya bahari, ilikuwa ikitafutwa, ambapo mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen aliongoza kikosi cha kutafuta manowari hiyo, na baada ya kupatikana kwake amesema kuwa  ugunduzi huo ni wa kutia moyo.

Meli hiyo ilizamishwa Julai 30, 1945 katika habari ya Ufilipino kati ya Guam na Leyte baada ya kugongwa na kombora kutoka kwa nyambizi ya Japan.

Kisa hicho kilielezwa kuwa kibaya zaidi cha kupotea kwa maisha kulikumba jeshi la wanamaji wa Marekani kwani ndani ya Manowari hiyo kulikuwa na wanajeshi 1,196 na ni kati ya wanajeshi 800 na 900 walinusurika kuzama.

Meli hiyo ni maarufu kwa kufanya safari ya siri ya kusafiirisha sehemu za kuunda bomu la atomic lililofahamika kama “Little Boy” .

Bidhaa hizo zilipelekwa katika kisiwa cha Tinian kwenye kambi ya jeshi la Marekani ambayo ilifanya shambulizi la kwanza na bomu la nyuklia.

 

Picha: Ziara ya Rais Dkt. Shein wilayani Magharibi A
Dkt. Shein aeleza anayefanya maamuzi ya CCM, akagua mradi wa visima