Mlinda Lango la Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Aishi Salum Manula ameendelea kuonyesha ubora wake kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo akiwa Msimbazi kwa kuweka rekodi mbalimbali.

Baada kutoruhusu bao katika mchezo dhidi ya KMC FC, Mlinda Lango huyo imefikisha ‘clean-sheet’ 17 kwa msimu huu akisaliwa na mchezo mmoja tu kuifikia rekodi yake ya misimu miwili iliyopita aliyomaliza ligi akiwa na 18.

Kama Manula atadaka michezo mitatu ya Ligu Kuu iliyosalia Msimu huu 2020/21 dhidi ya Coastal Union, Azam FC, na Namungo bila kuruhusu bao basi atavunja rekodi yake ya 2017/2018.

Pamoja na kwamba msimu huu huenda Manula atabeba ubingwa wa nne mfululizo akiwa na Simba SC, pia itakuwa kwa mara yake ya nne kuibuka kinara wa clean-sheets kwani hakuna kipa wa timu nyingine atakayefikisha cleensheets hizo kwa msimu huu.

Tangu Manula alipojiunga na Simba SC msimu wa 2017/2018 amekuwa akiimarika kila siku na kuwa kipa namba moja wa timu hiyo pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars na ameng’ara pia katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

Mourinho kufyeka wanane AS Roma
Waziri Kalemani azindua mradi wa PERI URBAN