Afarah Suleiman, Babati Manyara.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania, CP Awadhi Haji amesema hali ya ulinzi na Usalama Mkoani Manyara imeimarika, kwa ajili ya kilele Cha Mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 14 Oktoba, 2023 Mkoani humo.
Awadh ameyasema hayo hii leo Oktoba 13, 2023 kusema ulinzi wa Viongozi Wakuu wa Nchi na wageni wote umeimarishwa, ili kuhakikisha shughuli iliyokusudiwa inafanyika kwa utulivu na amani.
Amesema, Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Naibu waziri Mkuu na Viongozi wengine wa Serikali na chama watashiriki kilele hicho
Jumla ya Askari 900 kutoka mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma wanashiriki kuimarisha ulinzi Mkoani Manyara.