Maofisa wawili wanashikiliwa kwa tuhuma ya kuomba rushwa ya Tsh.Milioni 1 ili wamsaidie mama mmoja kupata nafasi katika shule ya Bweni kwaajili ya mwanaye.
Mkuu wa Takukuru Mwanza, Ernest Makale amesema maofisa hao ni Mugusi Isaya (59) ambaye ni ofisa kilimo na mazingira katika halmashauri ya jiji la Mwanza na Japhet Buchwa (58) ofisa elimu manispaa ya Ilemela
Maofisa hao walitenda kosa hilo Januari 31 mwaka huu.
“Fedha hizo zilipokelewa na Mugusi kutoka kwa Rosemary Makenke (57) ambaye ni Ofisa utamaduni Manispaa ya Ilemela ambaye ndiye alitumiwa kupitia simu yake ya mkononi,” amesema Makale.
Makale ameongezea kuwa baada ya kuwahoji watuhumiwa hao, walikiri kupokea kiasi hicho cha fedha na kisha kuandaa nyaraka feki ili aweze kumsaidia, Rhobi kumtafutia shule ya bweni mtoto wake huku akijua ni kosa kisheria na hana mamlaka ya kufanya hivyo.
Mugusi pia alikiri kuandaa nyaraka za uhamisho feki kwenda shule ya sekondari Old Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo baada ya kufika huko uongozi wa shule ulibaini nyaraka zilizoandaliwa ni feki hivyo kulazimika kurudi nyumbani.